ETHIOPIA-MAANDAMANO

Waandamanaji Ethiopia washambulia viwanda

Waandamanaji nchini Ethiopia wamefanya uharibifu katika viwanda na mashamba kadhaa yanavyomilikiwa na wageni ikiwa ni pamoja na magari kadhaa na kuongeza waathirika wa kiuchumi katika ghasia za kudai haki dhidi ya uvamizi wa ardhi.

Waandamanaji Oromo nchini Ethiopia wafanya uharibifu wa viwanda
Waandamanaji Oromo nchini Ethiopia wafanya uharibifu wa viwanda REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Takribani viwanda kumi na moja vya nguo viliteketezwa kwa moto hivi kaibuni katika mji wa Sebeta na magari sitini kwa mujibu wa ripoti za nchini humo.

Ghasia hizo zinakuja wakati huu ambapo taifa hilo limekabiliwa na ukosolewaji wa kimataifa na upinzani mkali juu ya namna mamlaka inavyoshughulikia maendeleo.

Maandamanao hayo yanakuja baada ya vifo vya watu 55 katika mkanyagano jumapili iliyopita baada ya polisi kusambaratisha waoromo jirani na jiji la Adis Ababa.

Hadi sasa idadi ya vifo mia nne hamsini vya wanaharakati wa haki za binadamu na upinzani vimeripotiwa,baada ya kuuawa tangu mwaka 2015.

Mtafiti mmoja raia wa Marekani aliuawa jumanne iliyopita baada ya waandamanaji kushambulia gari lake kwa mawe jirani na Addis Ababa.