UJERUMANI-NIGER-USHIRIKIANO

Angela Merkel ziarani Niamey: matarajio ya raia wa Niger

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel azuru Niger Oktoba 10, 2016.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel azuru Niger Oktoba 10, 2016. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Baada ya kuzuru mji wa Bamako siku ya Jumapili Oktoba 9, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa mjini Niamey Jumatatu hii Oktoba 10. Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Niger tangu ashikiliye wadhifa huo. Wananchi wa Niger wanatarajia mengi katika ziara hii.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mahamadou Issoufou mwenye ndiye atakayempokea Kansela wa Ujerumani baada ya kushuka kutoka katika ndege yake maalumu akitokea mjini Bamako nchini Mali. Katika ukumbi mkubwa wa Baraza la Mawaziri, matarajio ya viongozi wa Nigeryatatolewa kwa Kansela Angela Maerkel.

Kuna mambo manne ya yanayopewa kipaumbele, amesema Waziri wa Mambo ya Nje, madaraka na utawala bora, kilimo na usalama wa chakula, afya na elimu ya msingi. Angela Merkel hata hivya atazuru shule moja mjini Niamey ili kujionea mwenyewe vifaa vinavyohitajika ili Ujerumani isaidie.

Changamoto ya wahamiaji

Changamoto zingine kubwa: usalama na uhamiaji haramu ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na viongozi hawa wawili. Niger ni nchiambako wahamiaji kutoka mataifa mengi barani Afrika hupitia kwa kujaribu kuingia Ulaya.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la kimatatifa linalotetea wahamiaji (IOM) nchini Niger, kati ya wahamiaji 80 000 na 120 000 wanakisiwa kupitia Niger mwaka 2016. Nia ya serikali ya Niamey ni kupunguza wimbi la uhamiaji kuelekea Ulaya, amesema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Niger.