WHO

WHO yataka vinywaji vyenye sukari kutozwa kodi zaidi kukabili tatizo la Obesity

Mmoja wa washindani wa shindano la kupunguza unene nchini Marekani (Uzito uliopindukia).
Mmoja wa washindani wa shindano la kupunguza unene nchini Marekani (Uzito uliopindukia). REUTERS/Finbarr O'Reilly/File Photo

Shirika la afya duniani WHO, limezitaka nchi mbalimbali duniani kuanza kutoza kodi kubwa kwenye vinywaji vinavyotumia sukari, wakati huu wakipambana na tatizo la unene uliopindukia maarufu kama Obesity, likisema kuwa kufanya hivyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vinywaji vya sukari.

Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo haya ya shirika la afya duniani kuhusu vinywaji vyenye sukari, yamekuja wakati huu dunia ikijidhatiti kupunguza tatizo la uzito uliopindukia, ambapo kwa sasa mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo hilo.

WHO inasema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba utozaji wa kodi ya ziada kwa vinywaji vinavyotumia sukari kutsababisha kupunguza tatizo na watumiaji wa vinywaji hivyo hasa kwa kuongeza kodi kwa zaidi ya asilimia 20.

Kwa maneno mengine, nyongeza ya asilimia 20 itapunguza matumizi ya unywaji wa vimiminika vya sukari kwa zaidi ya asilimia 20, huku asilimia 50 ya nyongeza ya kodi, kutapunguza karibu nusu yake, shirika hilo limesema.

Wakati huo huo idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kisukari duniani imeendelea kuongezeka tangu mwaka 1980, kutoka watu 108 hadi watu milioni 422 mwaka 2014.

Ugonjwa wa uzito uliopindukia pamoja na kisukari umesababisha vifo vya watu milioni 1 na laki tano mwaka 2012, huku magonjwa yanayohusishwa na matumizi makubwa ya sukari na kupelekea watu kuugua kisukari ukisababisha vifo vya watu milioni 2 na laki 2.