NIGER-USALAMA

Vyombo vya usalama vyadhibiti hali ya mambo katika gereza la Koutoukalé

Gereza la Koutoukalé kilometa hamsini kutoka mjini Niamey, lilishambuliwa na kundi la watu wenye silaha, mapema asubuhi, Jumatatu hii Oktoba 17.
Gereza la Koutoukalé kilometa hamsini kutoka mjini Niamey, lilishambuliwa na kundi la watu wenye silaha, mapema asubuhi, Jumatatu hii Oktoba 17. AFP

Nchini Niger, mapigano yalitokea mapema Jumatatu Oktoba 17 asubuhi katika gereza la Koutoukalé, kilometa hamsini kutoka mji mkuu Niamey. Katika gereza hili lililo chini ya ulinzi mkali wanazuiliwa viongozi wakuu wa kijihadi waliokamatwa nchini Niger, lakini pia Mali na Nigeria. Shambulizi hili, kwa mujibu wa taarifa za awali, ni la kigaidi

Matangazo ya kibiashara

Baada ya shambulizi hili, hali ya utulivu imerejea karibu na gereza la Koutoukalé. Jaribio la kuwatorosha wafungwa wa kigaidi lilishindikana. Washambuliaji zaidi ya kumi waliokuja wakitokea kwenye mpaka wa Mali wakiwa kwenye pikipiki, walitimka, huku wakiacha mwili wa mmoja wao aliyeuawa na kikosi cha ulinzi wa taifa kabla ya kulipua mkanda wake uliokua umejaa vilipuzi.

Baada ya kuwasili asubuhi, washambuliaji walirusha risasi kwenye lango kuu la gereza la Koutoukalé wakitumia bunduki kubwa ya kivita aina ya M80. Lakini lango halikuboka, na watu hao wenye silaha hawakuweza kuingia ndani ya jela.

Hakuna mfungwa hata mmoja ambaye aliweza kutoroka na hali kwa sasa iko chini ya udhibiti wa kikosi cha ulinzi wa taifa. Idadi kubwa ya vikosi vya usalama imetumwa katika jela hilo. Ndege za kivita na helikopta za kijeshi zilitumika kwa kudhibiti hali ya mambo. Awali gavana wa jimbo la Tillaberi, alisema washambuliaji watakamatwa na wadhibitiwe vilivyo, kutokana na vifaa vinavyotumika katika operesheni hiyo.