LIBYA-USALAMA

Nchi jirani zapinga nchi za kigeni kuingilia kati nchini Libya

Agosti 28, Bunge la Libya lilipiga kura tena dhidi ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Agosti 28, Bunge la Libya lilipiga kura tena dhidi ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Parlement libyen/DR

Wajumbe kutoka nchi jirani za Libya walikusanyika tarehe 19 Oktoba katika mji wa Niamey ili kujaribu kuendeleza faili ya mgogoro nchini Libya. Wanaohusika na kukosekana kwa utulivu huo, ambao ni Niger, Chad, Tunisia, Algeria, Sudan na Misri wamezitaka pande zinazokinzana kufanya mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miaka mitano baada ya nchi za kigeni kuingilia kati nchini Libya, hali nchini humo bado ni tete. "Leo tunashuhudia mikasa mingi nchini Libya na ni ndio sababu itahitajika kuwakutanisha wadau wote ili kutafuta suluhu," amesema Waziri wa mambo ya Nje wa Chad Moussa Faki Mahamat .

Kwa kauli moja, nchi sita jirani zilizokutana mjini Niamey walionyesha mshikamano wao kwa Libya inayokumbwa na mgogoro. Nchi jirani zinahisi pia kuhusika na kukosekana kwa utulivu na hivyo kuzitolea wito pande zinazokinzana kuketi kwenye meza ya mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote. "Hakuna hoja ya nchi za nchi kuingilia kati mambo ya Libya, hakuna ufumbuzi wa kijeshi. Tunaomba serikali kuwa na umoja, ili kuwafikia wale ambao hawashiriki katika serikali hiyo," amesema Pierre Buyoya, mwakilishi wa Tume ya Afrika.

Utulivu nchini Libya ni kwa maslahi ya raia wake lakini pia majirani zake, amesema Martin Kobler, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa. "Ni kweli kwa wadau wote kukubali ushauri wa jumuiya ya kimataifa, lakini wanapaswa kufanya hivyo wenyewe, Hatuwezi kuamua kwa niaba yao, " Martin Kbler amekumbuka.