AFRIKA KUSINI-ELIMU

Makabiliano mapya yazuka katika vyuo vikuu nchini Afrika Kusini

Polisi yatumia mabomu ya machozi kwa kutawanya umati wa wanafunzi, Oktoba 20mbele ya Ikulu ya rais ya Afrika Kusini.
Polisi yatumia mabomu ya machozi kwa kutawanya umati wa wanafunzi, Oktoba 20mbele ya Ikulu ya rais ya Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Nchini Afrika Kusini, hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudiwa katika vyuo vikuu. Alhamisi hii Oktoba 20 maandamano mapya yamefanyika katika vyuo vikuu nchini humo. Mapigano kati ya wanafunzi na polisi yalitiokea katika mji wa Johannesburg hasa, katika mabweni ya kitivo maarufu cha Wits na mbele ya makao makuu ya serikali mjini Pretoria ambapo wanafunzi walikuwa wamekusanyika.

Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi wamekuwa wakiandama kwa mwezi mmoja sasa wakitaka wapewe kwa elimu ya juu ya bure. mzozo ulianza baada ya serikali kutangaza ongezeko la ada ya chuo kikuu kwa mwaka 2017.

"Hatutorudi nyuma," amesema kiongozi wa wanafunzi mbele ya makao makuu ya serikali mjini Pretoria. Walikua wanafunzi 200 waliokusanyika mbele ya Ikulu ya rais kwa kuomba madai yao.

Polisi ilitumia mabomu ya machozi kwa kutawanya umati wa wanafunzi waliokua wakiandamana. Baada ya masaa kadhaa ya kusubiri, wanafunzi alikataa kuwasilisha maombi yao kwa afisa wa serikali aliyokua amekuja kuwasilikiza. Wanaomba kusikilizwa na serikali. Siku ya Alhamisi, Waziri wa kwenye Ofisi ya rais Jeff Radebe alijikuta anagonga ukuta baada ya kuwataka wanafunzi hao kuwa watulivu. "Ofisi ya imetoa wito kwa wanafunzi ili kuokoa mwaka wa masomo. Tunaendelea kuwa na wasiwasi kuhusu kuzuka kwa vurugu katika baadhi ya vyuo vikuu nchini kote. "

Serikali imeunda tume ya kujadili kuhusu ufadhili wa elimu ya juu. Lakini tume hii itatoa ripoti yake mwakani. tayari baadhi ya watu mbalimbali wameanza kuilaumu serikali kutokua na utashi wa kupatia ufumbuzi suala hilo

Rais Jacob Zuma ambaye alifanya ziara kadhaa nje ya nchi mwezi huuhajazungumzia chochote kuhusu madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu, wala kuzungumzia vurugu zinazoendelea katika vyuo vikuu mbalimbali na maeneo kadhaa ya nchi hiyo.