SUDAN

Rais Omar al Bashir aishutumu Amnesty International kwa "uongo" dhidi ya jeshi lake

Rais  Omar al-Bashir wa Sudan (kulia)akiwa na rais Jacob Zuma wa  Afrika Kusini
Rais Omar al-Bashir wa Sudan (kulia)akiwa na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini RFI-Hausa/ Nura

Rais Omar al-Bashir jana Jumamosi amelishutumu shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty Inernational kwa kueneza "uongo" kuwa vikosi vya serikali ya Sudan vimekuwa vikitumia silaha za kemikali dhidi ya raia katika eneo lenye vita la Darfur.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, Amnesty ilisema katika ripoti kuwa vikosi vya Sudan vilitekeleza mashambulizi zaidi ya 30 yanayodhaniwa kuwa ya silaha za kemikali katika eneo la milima ya Darfur yaliyoua watu 250, ikiwa ni pamoja na watoto wengi.

Akijibu kwa mara ya kwanza shutuma za Amnesty Intenational wakati akiwahutubia wafanyakazi wa chama chake cha National Congress Rais Bashir amesema tuhuma hizo ni uongo mtupu.

Makundi ya haki yanashutumu vikosi vya Sudan kwa kuendelea kutumia silaha zinazodhaniwa kuwa za kemikali dhidi ya raia kwenye jimbo la Darfur na katika eneo lenye misitu la Jebel Marra kati ya mwezi Januari na Septemba.