GHANA-USALAMA-SIASA

Askari wa Ghana waonywa

Accra, mji mkuu wa Ghana, ambapo Ibrahim Mahama, ndugu wa rais John MAhama alipoendesha mkutano wa kisiasa.
Accra, mji mkuu wa Ghana, ambapo Ibrahim Mahama, ndugu wa rais John MAhama alipoendesha mkutano wa kisiasa. Wikimedia Commons

Jeshi la Ghana limechukua hatua za kinidhamu kwa askari ambao walitoa ulinzi kwa Ibrahim Mahama, ndugu wa Rais John Mahama, wakati wa mkutano wa kisiasa uliyofanyika Jumapili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Askari hawakuwa waliruhusiwa kutoa ulinzi kwa mfanyabiashara, kwa mujibu wa Kanali Aggrey Quashie, msemaji wa jeshi la Ghana.

Askari walitoa ulinzi kwa msafara wa Ibrahim Mahama ni sehemu ya kikosi cha askari wanaolinda taasisi za nchi na hawakupata maelekezo ya kuwa katika ulinzi wa ndugu wa rais wa nchi, kanali Quashie amesema.

jeshi limeanzisha uchunguzi kuhusu askari hao, kufuatia picha za mfanyabiashara Ibrahim Mahama zilizorushwa ambapo aanaonekana akizungukwa na "watu kadhaa wenye silaha za kivita, watu ambao walikua wamejidhatiti, " imeandikwa katika ukurasa wa Facebook wa radio ya taifa ya Ghana.

Shahidi mmoja amerusha ujumbe katika ukurasa wa Facebook, akidai kuwa kulikua pia na magari ya kivita katika ulinzi wa ndugu wa rais Mahama.