ERITREA-USALAMA

Marubani wawili wa Eritrea waegesha Ethiopia na kuomba hifadhi

Eneo la kumbukumbu la mashujaa katika mji wa Mekele, Ethiopia.
Eneo la kumbukumbu la mashujaa katika mji wa Mekele, Ethiopia. Nichole Sobecki / AFP

Nchini Ethiopia, marubani wawili wa ndege za Eritrea walitoroka na ndege zao Jumatano wiki hii asubuhi na kutua katika uwanja wa Makele, mji mkuu wa jimbo la Tigre, ambapo waliomba mara moja hifadhi.

Matangazo ya kibiashara

Luteni Mebrahtu Tesfamariam na Luteni Fishaye Afeworki waliondoka Jumatano saa 4 saa za Erutrea katika kambi ya kikosi cha anga mjini Asmara, mji mkuu wa Erytrea. Walitumia ndege ndogo ya mafunzo aiana ya Zlin 143L, iliyotengenezwa nchini Jamhuri ya Czech.

Lakini saa moja baadaye, waliwasilianamamlaka ya uwanja wa ndege wa Mekele, nchini Ethiopia, katika upande wa pili wa mpaka, na kuomba ruhusa ya kutua. Ruhusa ambayo walipewa, wakati ambapo, kwa mujibu wa shahidi mmoja, ndege moja ya kijeshi ya Ethiopia ilipaa angani kwa ajili ya kukabiliana na uwezekano wa tishio.

Maveterani

Kwa mujibu wa wenzetu kutoka kituo huru cha Radio Erena, maafisa hao wawili ni maveterani, ambao wana miaka mingi ya ya kazi hiyo. Afisa wa kwanza alijiunga na jeshi mwaka 1999 na alifundishwa kuendesha moja ya kivita aina ya Migs-29 ya Eritrea. Afisa wa pili alijiunga na jeshi la anga mwaka 2002, chanzo hicho kimesema.

Hii si mara ya kwanza marubani wa Eritrea kukimbilia nje ya nchi wakiwa na ndege zao. Marubani kadhaa wa helikopta, na hata rubani wa ndege ya rais na naibu wake, walikimbilia mafichoni nchini Saudi Arabia katika miaka ya hivi karibuni.

Itafahamika kwamba hali ya manung'uniko inaripotiwa katika mamlaka ya usafiri wa anga nchini Eritrea tangu kufungwa kwa mwanzilishi wake, Meja Habtezion Hadgu mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia ya kumuomba Rais Isaias Afewerki kulegeza udikteta nchini humo.