UFARANSA-TOGO-GHANA

Ziara ya Manuel Valls kuimarisha mahusiano na mataifa ya Afrika Magharibi

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ameanza ziara rasmi ya siku nne katika nchi tatu za Afrika Magharibi ambapo siku ya ijumaa amekutana na viongozi wa Togo mjini Lome mji mkuu wa nchi hiyo, na baadaye kuelekea Ghana na Cote d'Ivoire.

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls
Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara hiyo mjini Lome Manuel Valls amekutana na viongozi wa taifa hilo na kwa pamoja wamefanya tathmini ya kina kuhusu utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo yanayofadhiliwa na nchi ya Ufaransa nchini humo.

Aidha viongozi hao wameangazia kuimarishwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Togo, hii ikiwa ndio lengo la ziara hiyo kwenye mataifa hayo, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema.

Taarifa zaidi zinasema Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls, amepanga kuweka wazi hatua zilizopigwa mpaka sasa kuhusu ahadi zilizotolewa na serikali yake chini ya uongozi wake Francois Hollande na kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa kabla ya kufika mwisho wa muhula wa rais Hollande mwaka 2017, ili kufikia malengo ya mahusiano kati ya Ufaransa na Afrika.