COTE D'IVOIRE-MANUEL VALLS

Waziri mkuu wa Ufaransa aombwa kusaidia uchunguzi kuhusu mwanahabari Guy-Andre Kieffer

Guy-André Kieffer mwandishi wa habari aliyetoweka mjini Abidjan mwaka 2004
Guy-André Kieffer mwandishi wa habari aliyetoweka mjini Abidjan mwaka 2004 Reuters

Shirika la Waandishi wa habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF) na familia ya mwandishi wa habari mwenye uraia wa Ufaransa na Canada Guy-André Kieffer, aliyetoweka mjini Abidjan mwaka 2004, wamemwandikia barua ya wazi waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ili kushinikiza uchunguzi kuhusu kutoweka kwa mwanahabari huyo,wakati wa ziara yake nchini Cote D’Ivore leo Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua hiyo waandishi hao wamemwomba waziri mkuu Valls kufanya kila liwezekanalo wakati wa ziara yake ili uchunguzi wanao endelea nao upate ari mpya na tume ya majaji kutoka Ufaransa inayohoji watuhumiwa itekeleze kitakachobainika.

Miaka kumi na miwili imepita tangu kupotea kwa Kieffer, na Katika matukio kadhaa, Cote D’Ivore na Ufaransa zimeonesha dhamira zao za kawaida kuhusu kurejesha haki lakini uchunguzi wao umekuwa haujibiwi wameeleza.

 

Hapo jana akiwa ziarani nchini Togo, waziri Mkuu Valls ameipongeza nchi ya Togo kwa mabadiliko yenye mwelekeo sahihi,na kuahidi kuimarisha zaidi ushirikiano na mahusiano ya kibiashara  katika nchi inazozitembelea za Togo, Ghana na Cote d'Ivore.

Ziara ya waziri mkuu Valls inalenga kuzihakikishia nchi hizo ambazo zinahisi kusahauliwa na Ufaransa katika miaka michache iliyopita, kuwa itaziunga mkono katika mabadiliko ya kidemokrasia na kuimarisha mahusiano ya biashara.