CAR-UFARANSA-SANGARIS

Kikosi cha askari wa Ufaransa kuondoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari wa Ufaransa wa operesheni Sangaris katika kata ya PK5 mjini Bangui mwezi Februari 2016.
Askari wa Ufaransa wa operesheni Sangaris katika kata ya PK5 mjini Bangui mwezi Februari 2016. Issouf Sanogo/AFP

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, aliwasili Jumapili jioni Oktoba 30 mjini Bangui, nchini Jamhuri ya afrika ya Kati ili kutamatisha rasmi operesheni Sangaris inayotekelezwa na vikosi vyake. Operesheni ambayo ilifanikisha kukomesha mauaji nchini humo, lakini ilishindwa kuyadhibiti makundi ya watu wenye silaha yanayohujumu raia.

Matangazo ya kibiashara

Saa chache kabla ya Jean-Yves le Drian kuwasili mjini Bangui, mapigano makali yalishuhudiwa katika kata ya PK5, mjini Bangui, kata wanakoishi Waislamu wengi. Mapigano hayo yalikua kati ya makundi matatu hasimuna yalisababisha vifo vya watu wengi.

Mwishoni mwa wiki hii, machafuko mengine yalizuka katikati mwa nchi hii. Mashambulizi ya hapa na pale na ghasia vimeendelea kushuhudiwa katika wiki za hivi karibuni na hivyo kutokea kuendelea kutokea kila kukicha.

Inasemekana kuwa matarajio ya kuondoka kwa askari wa Ufaransa yamepelekea kukuwa kwa makundi ya waasi na kutuhumiwa kutochukua hatua mara moja kwa vitendo viovu vinavyoendelea kutekelezwa na makundi haya. Muda wa kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa haujaonekana kuwa umewadia lakini Ufaransa uko tayari kuwarejesha nyumbani askari wake kutokana na vita dhidi ya ugaidi katika Mashariki ya Kati, Sahel na katika ardhi ya Ufaransa.

Ufaransa itabakiza askari 350 katika mji wa Bangui na ndege zisio na rubani ambazo zitakua zikifanya upelelezi kwa niaba ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (Minusca). Idadi ya askari wa Ufaransa inawezwa kuongezwa kwa ombi la serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iwapo kutatokea tishio kubwa kwa usalama wake.


■ Maoni ya wananchi wa CAR kuhusu kuondoka kwa askari wa Ufaransa

Mwezi Desemba 2013, Ufaransa ilianzisha operesheni Sangaris nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Miaka miwili baadaye, operesheni hiyo inamalizika, huku kila mmoja miongoni mwa wakazi wa mji wa Bangui akitoa maoni yake. Baadhi wamesifu kazi nzuri iliyotekelezwa na kikosi cha askari wa Ufaransa na wengine wamekosoa namna askari hao walishindwa kuyatokomeza makundi ya watu wenye silaha yanayohatarisha maisha ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, hasa katika mji mkuu wa nchi hii.