AU-ABDALLA

Abdalla Hamdok achukua nafasi ya Carlos Lopes kwenye uongozi wa ECA

Carlos Lopes, Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Afrika (ECA) aliyejiuzulu.
Carlos Lopes, Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Afrika (ECA) aliyejiuzulu. RFI

Kufuatia kuondoka kwa Carlos Lopes Jumatatu Oktoba 31, Abdalla Hamdok atahudumu kama Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Afrika (ECA) kuanzia Jumanne hii tarehe 1 Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Abdalla Hamdok, raia wa Sudan kwenye nafasi ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Afrika (ECA).

"Bw Hamdok aliwahi kuwa Mchumi na Naibu Katibu Mtendaji wa ECA tangu mwaka 2011. Kabla ya hapo, aliendesha na kufanikiwa kutekeleza shughuli za Tume ya Uchumi ya Afrika (ECA) kuhusu urasibu wa maendeleo ya sera, NEPAD na ushirikiano wa kikanda, pamoja na utawala bora, " taarifa ya CEA ya tarehe 31 Oktoba imeeleza.

Carlos Lopes atafakari juu ya mustakabali wa Umoja wa Afrika

Baada ya miaka 28 katika Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na miaka minne kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (ECA), Carlos Lopes, Mchumi kutoka Guinea-Bissau, alitangaza Septemba 30 kwamba yuko mbioni kujiuzulu.

Wiki iliyopita, aliteuliwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, pamoja na watu wengine wanane kutoka nchi za Afrika, kutafakari juu ya mageuzi ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika.