BAN-SUDAN KUSINI

Ban amfuta kazi Kamanda wa kikosi cha UN Sudan Kusini

Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko mjini Juba, UNMISS, wakionekana kwenye picha wakati fulani walipotekeleza zoezi la kunyang'anya silaha mjni Juba, sasa wanakosolewa kushindwa kuwalinda raia
Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko mjini Juba, UNMISS, wakionekana kwenye picha wakati fulani walipotekeleza zoezi la kunyang'anya silaha mjni Juba, sasa wanakosolewa kushindwa kuwalinda raia UN Photo/Eric Kanalstein

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemfuta kazi Kamanda wa kikosi cha kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) Jenerali Johnson Ondieki.

Matangazo ya kibiashara

Moon amesema amechukua hatua hiyo baada ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya mapigano yaliyozuka mwezi Julai mwezi huu.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema wanajeshi hao walishindwa kuwasadia raia wa kawaida na wafanyikazi wa kutoa misaada.

Umoja wa Mataifa ulituma kikosi hicho mwaka 2011 kulinda amani nchini humo.

Umoja wa mataifa imekiri kuwa vikosi vyake vya kulinda Amani Sudani Kusini vimeshindwa kuwalinda raia katika mji mkuu wa Juba wakati wa mapigono baina ya pande mbili mwezi Julai mwaka huu, ambapo watu kadhaa waliouawa na maelfu wengine kulazimika kuyahama makazi yao.