UN-WAANDISHI WA HABARI

Wanahabari Ghislaine na Claude wakumbukwa wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupinga udhalimu dhidi yao

Wanahabari wa idhaa ya RFI Ghislaine Dupont na Claude Verlon, ambao waliuawa kaskazini mwa nchi ya Mali, kwenye mji wa Kidal.
Wanahabari wa idhaa ya RFI Ghislaine Dupont na Claude Verlon, ambao waliuawa kaskazini mwa nchi ya Mali, kwenye mji wa Kidal. RFI

Katika ripoti ya kushtua, shirika la umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, linasema kuwa kila baada ya siku tano, muandishi mmoja wa habari huuawa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inasema kuwa, katika kipindi cha muongo mmoja, jumla ya wanahabari 827 wameuawa wakati wakiwa kazini, amesema mkurugenzi wa shirika la UNESCO wakati akitoa tathmini ya ripoti yao.

Miongoni mwa maeneo hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi ni pamoja na nchi za Kiarabu ikiwemo Syria, Iraq, Yemen na Libya, huku eneo la bara la latin Amerika likifuatia, imesema ripoti iliyoangazia usalama wa wanahabari na hatari wanazokabiliwa nazo.

Katika hatua ya kushangaza, vifo vingi, karibu asilimia 59 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita 2006 na 2015 wameuawa wakiwa kwenye nchi zenye vita.

Katika kipindi hiki, jumla ya wanahabari 78 waliuawa mwaka 2013 wengi katika nchi za kiarabu.

Hata hivyo katika hatua ya kuchangaza, kutoka kutokuwa na kifo chochote cha mwandishi wa habari kwenye nchi za Ulaya mwaka 2014, mwaka jana jumla ya wanahabari 11 wameuawa.

Ripoti hii inasema kuwa waandishi wa habari wa ndani ndio wako hatarini zaidi ukilinganisha na wale wa vyombo vya kimataifa, ambapo asilimia 90 wameathirika.

Mwanahabari wa Iraq akimsaidia mmoja wa raia aliyenusurika kufa kutokana na shambulio la kundi la Islamic State mjini Mosul.
Mwanahabari wa Iraq akimsaidia mmoja wa raia aliyenusurika kufa kutokana na shambulio la kundi la Islamic State mjini Mosul. REUTERS/Goran Tomasevic

Hata hivyo jumla ya wanahabari 17 wa vyombo vya kimataifa waliuawa kwenye mwaka 2014, ukilinganisha na wanahabari wa nne miaka iliyopita.

Ripoti imebaini kuwa ni mara kumi zaidi wengi ni wanaume ndio wanaouawa ukilinganisha na wanawake, mfano mwaka 2014/15 wanaume wanahabari waliouawa walikuwa 195 huku wanawake ni 18.

Ripoti hii iliombwa na nchi wanachama 39 wa UNESCO.

Siku ya kimataifa ya usalama wa wanahabari na kupinga udhalimu dhidi yao, iliazimiwa na baraza la usalama la umoja wa Mataifa, ambapo kila ifikapo tarehe 2 ya mwezi Novemba kila mwaka, waandishi wa habari waliouawa wakiwa kazini hukumbukwa.

Siku hii ilianzishwa mahsusi mara baada ya mauaji ya kikatili ya wanahabari wawili wa shirika la utangazaji la Ufaransa RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kuuawa kaskazini mwa nchi ya Mali kwenye mji wa Kidal.