NIGER-USALAMA

Niger: watu 38 wakamatwa baada ya vifo vya wanakijiji 18

Picha ya wafugaji wako katika hali ya mvutano katika jimbo la Agadez, kaskazini mwa Niger.
Picha ya wafugaji wako katika hali ya mvutano katika jimbo la Agadez, kaskazini mwa Niger. Getty Images/ Aldo Pavan

Nchini Niger, watu 38, wengi wao wakiwa vijana wakulima , walikamatwa na polisi baada ya vifo vya wanakijiji 18 Jumanne wiki hii. Mapigano yalizuka kati ya wakulima na wafugaji karibu na wilaya ya Bangui, mkoani Tahoua magharibi mwa nchi. Mapigano ambayo pia yalisababisha watu zaidi ya 40 kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Yote yalianza Jumanne asubuhi wakati ng'ombe waliposhambulia shamba la nafaka. Katika mabishano yaliyofuata mmiliki wa shamba aliuawa. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema kuwa kulitokea 'purukushani'. 'Purukushani' kati ya wakulima na wafugaji kutoka jamii ya Peul ambazo zilisababisha vifo vya watu 18, ikiwa ni pamoja na 7 waliochomwa moto wakiwa hai, wakiwemo wanawake, watoto na wazee, wengine 43 wakijeruhiwa na nyumba 22 kuchomwa moto. Wanawake na watoto mia moja na ishirini na tatu waliotishiwa na wauaji waliwekwa haraka chini ya ulinzi wa polisi.

Migogoro hii inatokea mara kwa mara nchini Niger, hasa wakati wa kipindi cha mavuno ambayo pia kinaendana sanjari na kipindi cha kupeleka mifugo katika maeneo makubwa ya malisho.

Migogoro ya kijamii

Kile kinachotajwa kuwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ni mgogoro ya kijamii ambao umekithiri, kila wakati waathirika ni wale wake, watu kutoka jamii ya Peul, wawe wakulima au la.

Mashirika ya haki za binadamu yamekosoa tabia ya viongozi ya kusalia kimya na kutochukua uamuzi wa kukomesha migogoro hii.

"Mwanzoni, ilionekana kuwa ni mgogoro kati ya wakulima na wafugaji, lakini inapokithiri, mtu wowote kutoka jamii ya Peul na yule anayefanana na watu kutoka jamii hii hushambuliwa. Watu walishambuliwa, waliuawa, walichomwa moto kwa misingi yakutoka katikajamii fulani. Fikiria watoto ambao walikua ndani ya nyumba zao nyumba hizo zikiteketezwa kwa moto. Mimi nanyosha kidolea cha lawama kwa viongozi wa nchi hii, " amesema Harouna Abarchi, afisa wa ufugaji na mazingira katika shirika la ufugaji nchini Nigeria.