UN-MABADILIKO YA TABIA NCHI

Tabia nchi: Utata waendelea siku chache kabla ya kuanza kwa utekelezwaji wa mkataba wa Paris

Watu wakitazama picha ya mfano wa hali ya joto duniani
Watu wakitazama picha ya mfano wa hali ya joto duniani Reuters/路透社

Siku chache zikiwa zimesalia kabla ya makubaliano ya jijini Paris kuanza kutekelezwa, wanadiplomasia wa kimataifa ambao wanakutana Jumatatu ya terehe 7 jijini Marrakesh, wanakabiliwa na shinikizo la kutafsiri makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kama sehemu ya kuokoa dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kukabiliana na uharibifu wa tabaka la hewa, kumepelekea dunia kuwa kwenye hali ya hatari zaidi, ambapo joto limezidi kuongezeka maradufu, hali inayoweka makubaliano ya Paris kutofikiwa kwa wakati.

Mjadala kuhusu namna ya kutawanya dola za Marekani milioni 100 kwa mwaka kwa nchi ambazo zimeathirika na mabadiliko ya tabia nchi umeendelea kuwa mkali na mgumu licha ya ripoti mpya kuonesha kuwa kiasi hicho kinapaswa kuongezwa katika kipindi cha miaka 15 ijayo.

Mbali na mjadala huu, swali kubwa linalobaki na kuumiza wengi, ni ikiwa mgombea wa chama cha Republican Donadl Trump atashinda kiti cha urais wa Marekani, mgombea ambaye dunia inamuona adui wa mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi.

Wadadisi wengi wa mambo wanaona kuwa ushindi kwa Trump ni sawa na kuzika makubaliano ya Paris, makubaliano ambayo mgombea huyo ameshatangaza kuwa atayafuta kwa nchi yake.

Wengi wa wanadiplomasia wanaoshiriki mkutano wa safari huu, wangependa zaidi kuona mgombea Hillary Clinton anashinda kiti cha urais, kwa kile wanacho amini kuwa utekelezaji wa mkataba wa Paris utakuwa wa uhakika.