SOMALIA - USALAMA

Shambulizi nje ya bunge Mogadishu laua wanajeshi wawili

Wanamgambo wa Al Shabab wa Somalia
Wanamgambo wa Al Shabab wa Somalia

Takribani wanajeshi wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililolenga gari jirani na bunge la Somalia mjini Mogadishu,polisi wameeleza.

Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ambao ulilenga msafara wa wanajeshi jirani na eneo la makutano ya Sayidka unadaiwa kutekelezwa na wanajihadi wa kiislamu Alshabab.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters Polisi wametaja wanajeshi wawili waliuawa na wengine watano walijeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa katika eneo lililokuwa na polisi wanajeshi na wanausalama wengine.

Imebainishwa kuwa mshambuliaji ambaye nae aliuawa alikusudia kuua wanausalama wengi mpango ambao alishindwa na kushambulia gari moja iliyokuwa na askari kadhaa.