CAR-COTE D'IVOIRE

Rais Touadéra ziarani Cote d' Ivoire

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara akimpokea mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra mjini Abidjan, Novemba 7, 2016.
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara akimpokea mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra mjini Abidjan, Novemba 7, 2016. REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati yuko ziarani nchini Cote d'Ivoire tangu Jumatatu hii Novemba 7. Alipokelewa kwenye uwanja wa ndege na mwenyejio wake Alassane Ouattara.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ni yenye maslahi mengi, ikiwa ni pamoja na kutafuta msaada kutoka Cote d'Ivoire katika hatua za mbeleni za ujenzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini pia kujifunza kutokana na hali ya iliyotokea nchini humo, na hatimaye kutafuta wafadhili, kwa kuanzia benki ya Afrika kwa ajili ya maendeleo (ABD).

Ziara ya Rais Faustin-Archange Touadera ina malengo mawili: kwanza, kutafuta msaada wa kifedha na pia kujifunza yale uzoefu wa wa hivi karibuni wa Cote d'Ivoire ambao bado unatumiwa hadi leo kwa ujenzi wa nchi hiyo iliyokumbwa na muongo mmoja wa mgogoro na kupatanisha pande zilizokuwa zikihasimiana.

"Tutaanza mchakato wa kupokonya raia silaha na kuboresha maridhiano ya kitaifa, mshikamano wa kijamii, amesema Faustin-Archange Touadéra baada ya kukutana na Alassane Ouattara. Raia wa Cote d'Ivoire pamoja na hali iliyowakabili waliweza kuafikiana na kukomesha uhasama uliyokua ukiwakabili. Tunataka kujifunza kutoka kwa Cote d'Ivoire njia waliyotumia kwa kufikia maendeleo. "

Wasiwasi mwingine kwa raia wengi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ni kuondoka kwa kikosi cha askari wa Ufaransa wa Sangaris nchini mwao. "Tulitaka kikosi hiki kibaki, lakini kwa masuala ya ndani, nadhani kwamba Ufaransa iliamua kuondoa kikosi hiki cha Sangaris, lakini walituhakikishia kwamba askari kati ya 200 na 300 watabaki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na hivyo watashirikiana na kikosi cha Umoja wa Mataifa (Minusca). Lakini pia kuna kitengo cha kiufundi cha ndege zisio na rubani ambacho kitatumwa ifikapo mwezi Januari mwakani ili kuendelea kulinda raia, " Rais Touadara amesema.