LIBERIA-MAREKANI

Sirleaf asikitishwa na kushindwa kwa Hillary Clinton

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf REUTERS/Lucas Jackson/Files

Katika pongezi za Wakuu wa nchi za Afrika kwa ushindi wa Donald Trump, Rais wa Liberia ameonekana kiongozi wa kwanza kuonyesha masikitiko yake kufuatia kushindwa kwa Hillary Clinton katika uchaguzi wa uraiswa Marekani.

Matangazo ya kibiashara

"Nimesikitishwa sana kuona Bi. Clinton anakosa fursa hii kwa upande wa raia wa Marekani kwa kujiunga katika mfumo huu mdogo wa kidemokrasia kwa kukomeshwa kitendo cha kubaguliwa kwa wanawake," amesema Ellen Johnson Sirleaf katika mahojiano na BBC.

"Hata hivyo, Liberia imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Marekani. Na tunatarajia kwamba uhusiano huu mzuri utadumu," ameongeza Bi Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika mfumo wa kidemokrasia katika uongozi wa nchi barani Afrika.

Alipoulizwa kuhusu hatma ya baadaye kuhusu mahusiano kati ya utawala Trump na Afrika, Rais wa Liberia alijibu akisema kuwa ni mapema mno kutoa maoni yake juu ya swali hilo.

"Itabidi kusubiri na Tuone. Ni wazi kwamba tuna wasiwasi, lakini tunapaswa kumpa nafasi ili aweze kujifikiri katika sera zake," Sirleaf amesema.