DRC-UNSC-USALAMA

Ujumbe wa Baraza la Usalama la UN wasubiriwa mjini Kinshasa

Nchini DRC, ujumbe wa wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwasili Ijumaa hii Novemba 11 mjini Kinshasa hadi Novemba 14.

Jumamosi Novemba 12, ujumbe wa Baraza la Usalama la wa Mataifa utakutana na Rais Joseph Kabila.
Jumamosi Novemba 12, ujumbe wa Baraza la Usalama la wa Mataifa utakutana na Rais Joseph Kabila. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Lengo la ziara hii ya siku 3 katika mji mkuu wa DRC na katika mji wa Beni kaskazini mwa nchi ni kupunguza joto la kisiasa lililoshuhudiwa wiki za hivi karibuni wakati ambapo unakaribia mwisho wa muhula wa pili wa Joseph Kabila ifikapo mwezi Desemba mwaka, hasa marufuku ya kuandamana katika mji mkuu Kinshasa na kuzimwa kwa mitambo ya RFI tangu siku 6 zilizopita.

Ujumbe wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa, ni ishara kubwa. Hasa katika wakati huu wa mwaka ambapo mabalozi wa Umoja wa Mataifa hawana kawaida ya kusafiri.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni njia ya kuonyesha kuwa jumuiya ya kimataifa inaufuatilia mgogoro wa kisiasa nchini DRC kwa umakini, inataka ufumbuzi wa amani upatikane.

Watu wengi wamekua wakijiuliza ni ahadi gani ujumbe huu utapata kutoka pande husika? Hili ni tatizo kubwa kwani nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wote hawakubaliani kuhusu ujumbe watakaowafikishia wahusika.

Kama Marekani, Ufaransa na Uingereza watapendelea kupata ahadi kutoka kwa Joseph Kabila kwamba hatawania katika uchaguzi wa urais, na kwamba uchaguzi huo uahirishwe hadi mwaka 2017, nchi kama Urusi, China wanafikiria kuwa ni kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi iliyohuru. Nchi hizi mbili zinataka kukaribishwa kwa makubaliano ya kisiasa yaliyoafikiwa na kutiliwa sainimjini Kinshasa tarehe 18 Oktoba kati ya serikali na kundi moja la vyama vya upinzani.

Kuna uwezekano kuwa mabalozi wa Umoja wa Mataifa wakajizuia kuchukua hatua kali na kuwataka tu wadau wote nchini DRC kushiriki uchaguzi uliyohusru na wenye uwazi na kujiepusha na machafuko mapya kama yale yaliyotokea mwezi Septemba uliyopita.

Jumamosi Novemba 12, ujumbe wa Baraza la Usalama la wa Mataifa utakutana na Rais Joseph Kabila na Waziri wa Mambo ya Nje Raymond Tshibanda.