Habari RFI-Ki

Wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana na wadau wa siasa DRC

Sauti 09:44
Rais wa DRC, Josephu Kabila
Rais wa DRC, Josephu Kabila DR

Nchini DRC, ujumbe wa wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwasili Ijumaa hii Novemba 11 mjini Kinshasa hadi Novemba 14.Lengo la ziara hii ya siku 3 katika mji mkuu wa DRC na katika mji wa Beni kaskazini mwa nchi ni kupunguza joto la kisiasa lililoshuhudiwa wiki za hivi karibuni wakati ambapo unakaribia mwisho wa muhula wa pili wa Joseph Kabila ifikapo mwezi Desemba mwaka, hasa marufuku ya kuandamana katika mji mkuu Kinshasa na kuzimwa kwa mitambo ya RFI tangu siku 6 zilizopita.