TABIA NCHI

Ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yapongeza udhibiti wa gesi ya Carbon

Ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabia nchi imeonesha kuwa, udhibiti wa gesi ya Carbon inayotokana na uchomaji wa nishati ya mabaki ya mimea na wanyama, imeweza kudhibitiwa kwa kiwango kisichobadilika kwa miaka mitatu mfululizo, lakini ikaonya kuwa bado juhudi zaidi zinahitajika kuzuia ongezeko la joto duniani.

Mnara wa Eiffel jijini Paris, uliotumika kuashiria kufikiwa kwa makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Mnara wa Eiffel jijini Paris, uliotumika kuashiria kufikiwa kwa makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imesema kuwa, udhibiti wa hewa ya ukaa (carbon dioxide) ulibakia kwenye kiwango kisichobadilika mwaka 2015 ambapo kilikuwa ni tani bilioni 36.3 (GtCO2) na kilitarajiwa kuongezeka angalau kwa asilimia 0.2 mwaka 2016.

Mtafiti Corinne le Quere kutoka chuo cha east Anglia aliyeshiriki kuandika ripoti ya bajeti ya kupambana gesi ya Carbon, amesema kuwa "huu ni mwaka watatu hakujashuhudiwa ongezeko lolote la hasa katika kipindi hiki ambacho uchumi wa dunia umeendelea kukua."

Wataalamu hao wamesema kuwa, hali hii imechangiwa na kupungua kwa matumizi makubwa ya makaa ya mawe na nchi ya China, na kwamba hii ilikuwa ni ishara tosha ya "kufikia malengo" wakati huu kasi zaidi ikihitajika kupunguza matumizi ya gesi zinazotokana na uchomaji wa mimea na wanyama.

Wataalamu hao wanasema kuwa kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2013 kiwango kilikuwa ni asilimia 2.3 lakini kikapungua kwa kiwango kikubwa kwa asilimia 0.7 mwaka 2014.

"Huu ni msaada mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini haitoshi," alisema Le Quere.

Kwa dunia ili kufikia malengo kati audhibiti wa kiwango cha wastani wa hali ya joto duniani angalau kwa nyuzi joto 3.6, basi ni lazima nchi zifanye kupunguza matumizi ya gesi za Carbon kwa kiwango zaidi ya hicho.

Kupungua kwa nyuzi joto kwa wastani wa asilimia 0.9 kwa mwaka ndio malengo yaliyowekwa kidunia hadi kufikia mwaka 2030.

Uharibifu wa tabaka la hewa umeendelea kuongezeka, ripoti hii imeonya, ambapo sasa inakadiriwa imefikia kiwango cha tani 23 za GtCO2 mwaka uliopita na kinatarajiwa kufikia tani 25 mwaka 2016.