MABADILIKO TABIA NCHI-MARRAKESH

UN: Mataifa tajiri yatoe fedha kwa nchi zinazoendelea, kukabili mabadiliko ya tabia nchi

Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, Patricia Espinosa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar, November 12, 2016.
Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, Patricia Espinosa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar, November 12, 2016. REUTERS/Youssef Boudlal

Umoja wa Mataifa, UN, umetoa wito kwa mataifa tajiri duniani kuhakikisha yanatoa  fedha zaidi ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Matangazo ya kibiashara

Uwezeshaji wa kifedha ni suala mtambuka kwenye mazungumzo ya umoja wa Mataifa yanayoendelea mjini Marrakech, Morocco, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mataifa kufikia makubaliano yaliyoanza muda mrefu jijini Paris mwaka uliopita, kwa lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani linalosababishwa na uchomaji wa mabaki ya mimea na wanyama.

Mataifa tajiri yaliahidi mwaka 2009, kuwa yangechangisha kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa mwaka, kuanzia mwaka 2020 kama msaada kwa nchi zinazoendelea ili zikabiliane na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hata hivyo nchi masikini bado zinataka kupatikana kwa njia bora zaidi ya kufikia malengo hayo, na hasa kwenye suala la fedha na utekelezaji, masuala ambayo ndio yatakayotoa dira ya vita yenyewe ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mpaka sasa, licha ya utekelezaji wenyewe kuanza, kiasi kilichotolewa hadi sasa ni chini ya nusu ya kiwango ambacho kimekubaliwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar akiwa na waziri wa mazingira wa Ufaransa, Ségolène Royal, Novemba 7, 2016
Waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar akiwa na waziri wa mazingira wa Ufaransa, Ségolène Royal, Novemba 7, 2016 REUTERS/Youssef Boudlal

"Gharama kwa nchi zinazoendelea kuweza kutekeleza mpango wenyewe, utazigharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 140 hadi bilioni 300 hadi kufikia mwaka 2030, na kuanzia dola bilioni 280 hadi dola bilioni 550 hadi kufikia mwaka 2050, ikiwa ni mara tano zaidi ya vile ambavyo ilikadiriwa," limesema shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira.

"Dunia iliahidi kuzisaidia nchi zinazoendelea ili zifikie leo kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi, hasa mabadiliko ya mvua na kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari," ameongeza mkuu wa shirika hilo, Erik Solheim.

"Lazima tutimize ahadi zetu, na lazima tupunguze utofauti wa upatikanaji wa fedha za utekelezaji ili kuhakikisha kuwa hakuna tofauti kubwa sana baadae, na ni kwakuongeza michango yetu mara mbili zaidi," alisema Solheim.

Kwa mujibu wa shirika la uchumi na maendeleo, OECD, ahadi zilizotolewa na nchi tajiri katika mwaka 2015 peke yake, kutaongeza mchango wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 41 mwaka 2014 hadi 2014 na kufikia dola bilioni 67 mwaka 2020.

Mkataba wa kimazingira uliokubaliwa jijini Paris mwaka uliopita, uliweka malengo ya kuhakikisha dunia inapunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 2 kwa nchi za viwanda na hasa kwa kupunguza matumizi ya hewa ya ukaa inayotokana na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi.

Kwaajili ya kufikia lengo hili, nchi zinazoendelea zinahitaji msaada mkubwa wa kifedha unahitajika ili kuzifanya nchi hizi ziondokane na matumizi ya gesi zinazotokana na wanyama na mimea, na kuhamia kwenye matumizi ya nishati mbadala.