ICC-SHERIA

Fatou Bensouda akosoa mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Afrika

Fatou Bensouda wakati wa kuapishwa kwake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini Hague tarehe 15 Juni 2012.
Fatou Bensouda wakati wa kuapishwa kwake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini Hague tarehe 15 Juni 2012. AFP

Nchi zilizotia sani kwenye makubaliano ya Roma yaliyopelekea kuundwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) zinakutana tangu Jumatano hii. Mkutano hu utadumu kwa wiki moja mjini Hague, nchini Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni mkutano unaofanyiia kila mwaka ambao unazishirikisha nchi anachama wa Mahakama hiyo. Lengo la mkutano huu ni kutathmini shughuli za Mahakama na kuidhinisha bajeti yake. Lakini mwaka huu mkutano huu unafanyika katika mazingira tete tangu nchi tatu za Afrika9 Burundi, Afrika Kusini na Gambia) kutangaza nia yao ya kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Wakati wa mkutano wa nchi wanachama, Mwendesha Mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda amesema kuwa baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika hawataki wanyooshewe kidole kwa makosa wanayotekeleza, huku wakipinga Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ili wasiweze kufuatilia. Hata hivyo amesema kusikitishwa na uamuzi wa kujiondoa kwa baadhi ya nchi za Afrika katika makubaliano ya Roma yaliyopelekea kuundwa kwa mahakama hiyo. Kwa mujibu wa Fatou Bensouda uamuzi wa viongozi hao unaitenga dunia katika ulimwengu wenye sheria, kwenye lengo la sheria kwa wote.

Bila shaka, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imeendelea kuwa na wasiwasi tangu kukosolewa na nchi kadhaa kutoka afrika ambazo zinaituhumu kwamba uamuzi wake huchukuliwa kutoka kwa nchi za magharibi. Hayo yanajiri wakati Mahakam hio iliituhumu Marekani Jumanne wiki hii kwamba ilitekeleza uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

"Msiondoke"

Mwenyekiti wa Baraza la nchi wanachama wa Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Waziri wa Sheria wa Senegal, alituma ujumbe kwa nchi hizi tatu: akizitaka 'kutojiondoa'. "Tumesikia madai yenu, ni halali. Ni lazima tutafutiye ufumbuzi mgogoro huu. "

Kwa upande wake, Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad al-Hussein alizungumzia masikitiko yake, lakini akasema kujiondoa kwa nchi hizi ni njia tu ya kulinda viongozi wa nchi hizo dhidi kufunguliwa mashitaka. Amesisitiza hasa nchi kadhaa za Afrika miongoni mwa 34 ambazo zingependa kuendelea kuwa wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).