GLOBAL WITNESS-DRC

Global Witness yahoji uuzwaji wa haki zote za shirika la madini nchini DRC

An open pit gold mine at the Kibali mining site in northeast Democratic Republic of Congo
An open pit gold mine at the Kibali mining site in northeast Democratic Republic of Congo Reuters

Shirika la madini la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetia saini kutoa haki zote za uchimbaji wa madini ya shaba kwa kampuni ya mtu ambaye ni rafiki wa karibu wa Rais Joseph Kabila, imeonesha ripoti ya taasisi ya Global Witness.

Matangazo ya kibiashara

Global Witness, taasisi isiyo ya kiserikali inayopambana na rushwa, mazingira na ukiukwaji wa haki, imesema kuwa shirika la Gecamines limetia saini kuidhinisha haki miliki kutoka kampuni ya Uswis ya madini Glencore kwaajili ya mradi wa uchimbaji wa madini ya shaba kusini mashariki mwa nhci hiyo, ambapo sasa kampuni iliyopewa haki hiyo imefahamika kama Africa Horizons Investment Limited.

Kwenye ripoti yake, taasisi hiyo imesema kuwa, mkataba uliotiwa saini mwezi Januari mwaka 2015, hauelezi ni kiasi gani ambacho shirika la madini la Kongo litakuwa linapokea kutokana na faida ya uchimbaji wa madini hayo, kutoka kwenye mgodi wa Kamoto.

"Haki miliki hiyo huenda ikazalisha kiasi cha zaidi ya dola za Marekani milioni 880, ikiwa ni zaidi ya kiasi ambacho kimetengwa kwenye bajeti ya afya ya nchi hiyo," limesema shirika la Global Witness.

Kampuni ya Africa Horizons inamilikiwa na bilionea wa kiyahudi, Dan Getler, bilionea ambaye taasisi ya Global Witness inasema kuwa amekuwa akihusishwa na mikataba mibaya ya uchimbaji madini nchini DRC na ni rafiki wa karibu wa Rais Kabila.

"Inasikitisha kuona shirika la uma limetoa haki zote kwa kampuni hiyo, ambapo ni sawa na kutoa kiasi chote cha fedha ambazo zingeweza kutumika kuijenga nchi ya DRC," amesema meneja wa kampeni wa shirika hilo, Pete Jones.

Jones ameongeza kuwa, mkataba huo hautoi sababu yoyote ya kwanini shirika la uma la Gecamines limeamua kutoa haki zote kwa kampuni ambayo haijulikani.

Ripoti ya Global Witness inatolewa wakati ambapo juma hili, Rais Joseph Kabila wakati akihutubia wabunge na wawakilishi wa seneti, alisema kuwa sekta ya madini imeendelea kuimarika na kwamba fedha zinazoendelea kupatikana zitatumika kuijenga nchi hiyo.