COTE D'IVOIRE-SIMONE GBAGBO

Kesi ya Simone Gbagbo kuendelea bila mtuhumiwa kuwepo

Simone Gbagbo akisikilizwa mahakamani Juni 1, 2016 mjini Abidjan, Cote d'Ivoire.
Simone Gbagbo akisikilizwa mahakamani Juni 1, 2016 mjini Abidjan, Cote d'Ivoire. ISSOUF SANOGO / AFP

Kesi ya Simone Gbagbo, aliyekuwa mke wa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, anayeshtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu, itaendelea bila ya mtuhumiwa kuwepo pamoja na wanasheria wake, jaji mkuu Boiqui Kouadio ameamua Jumatano hii Novemba 16.

Matangazo ya kibiashara

Simone Gbagbo kwa mara nyingine tena Jumatano hii amekataa pamoja na wanasheria wake kuripoti mahakamani. Baada ya Mwendesha mashitaka pamoja na upande wa walalamikaji kusikilizwa, jaji mkuu Boiqui Kouadio amesema kuwa inawezekana kuendelea na kesi biala ya kuwepo kwa mtuhumiwa.

Amewapiga marufuku wanasheria kadhaa wa Simone Gbagbo kuendelea kumsimamia mteja wao na kuamua kesi hiyo kusikilizwa tarehe 28 Novemba 2016.

Wanasheria wa Simone Gbagbo walisitisha kushiriki katika kesi hiyo "kutokana na mwenendo wa Mahakama, ambayo inakataa kuwaitisha mahakamani mashahidi wanaohitajika ili kujua ukweli," wakili Habiba Toure, moja wanasheria wa Simone Gbagbo amesema.

Miongoni mwa watu wanaotakiwa na upande wa utetezi kusikilizw mahakamni ni pamoja na Spika wa sasa wa Bunge na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro; Waziri Mkuu wa zamani Jeannot Kouadio Ahoussou; aliyekuwa Waziri Charles Koffi Diby; mkuu wa zamani wa majeshi, jenerali Philippe Mangou, na Mkuu wa polisi, Brindou M'Bia.

"Hakuna Ibara yoyote inayoeleza kuwa mwendesha mashitaka anapaswa kumuitisha mtuhumiwa mahakamani. Inaonekana kuwa mtuhumiwa hana uwezo wa kuitisha mashahidi wake, haiwezekani kumuomba mtu mnayeshitakiana kuwaleta mashahidi wake ili waje wakutetee, " Mwanasheria Mkuu Aly Yeo alijibu Novemba 2, wakati kesi hiyo ilikua tayari imefungwa.

Simone Gbagbo aliripotimahakamani Mei 31 mjini Abidjan kwa 'uhalifu dhidi ya wafungwa wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.'