ITALIA-LIBYA-MSF

Boti yazama Mediterranean: watu saba wafariki na mamia kukosekana

Wahamiaji wanaendelea kukumbwa na matatizo mbalimbali wanapojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean ili kuingia Ulaya.
Wahamiaji wanaendelea kukumbwa na matatizo mbalimbali wanapojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean ili kuingia Ulaya. ARIS MESSINIS / AFP

Ajali hii iliyotangazwa na Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) ni miongoni mwa mfululizo wa matukio mengine ambayo tayari yamesababisha vifo vya watu 11 na wengine 230 kukosekana Jumatatu na Jumanne katika wiki hii katika pwani ya Libya.

Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji saba wamekufa na mamia wengine hawajulikani walipo baada ya ya meli waliokuwemo kuzama katika pwani ya Libya, limetangaza Alhamisi hii Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), ambalo limewaokoa waathirika 27 na kuwasafirisha kwenye boti lake linalojulikana kwa jina la Bourbon Argos.

"Watu 27 wanaosafirishwa kwa sasa kwenye boti la Bourbon Argos walikuwa kwenye boti lililokua likibeba watu 130. Watu hawa ndio wamenusurika. Ajali hii ni mbaya mno," MSF imetangaza kwenye Twitter, na kusema pia wamefanikiwa kupata miili saba ya watu waliokufa maji.

Watu 3,200 waokolewa tangu Jumamosi

Haiwezekana kupata ufafanuzi wa haraka wa ajali hii mpya, ambayo ni miongoni mwa mfululizo wa matukio mengine ambayo tayari yamesababisha vifo vya watu 11 na wengine 230 kukosekana Jumatatu na Jumanne wiki hii katika pwani ya Libya.

Tangu Jumamosi, zaidi ya watu 3,200 waliokolewa kwenye boti zilizozama katika eneo hilo, kulingana na idadi iliyotolewa na kikosi cha ulinzi wa baharini kutoka Italia kinachoratibu shughuli hiyo.