MALAWI-SHERIA

Mwathrika wa ukimwi ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela

© Getty Images

Nchini Malawi, mwathirika wa ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kufanya kazi ngumu baada ya kukutwa na hatia ya kuhatarisha maisha ya watu, kwa kuwaambukiza kwa makusudi virusi vya ukimwi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa kukamatwa kwake, Eric Aniva, amekiri kuwa alijamiana bila kinga na wajane kadhaa. Amesema alikua na tumaini ya kuwatakasa, kitendo kiliyopigwa marufuku nchini Malawi.

Pia amebaini kwamba aliwanajisi wasichana takriban 100 baada ya hedhi yao ya kwanza, mila ambayo bado imeendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi ya Malawi.

Eric Aniva amesema kuwa alifanya ngono na wanawake zaidi ya mia moja bila hata hivyo kuwaeleza kuwa ni mwathirika wa ukimwi.

Kesi hii imewaghadhabisha watu wengi nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na mashirika ya haki za binadamu, hasa mashirika yanayotetea haki za wanawake na wasichana nchini humo.