EQUATORIAL GUINEA-GHUBA

Morocco yajiondoa kwenye mkutano wa Malabo kwa sababu ya Sahara Magharibi

Wakuu wa nchi za Afrika na zile za kiarabu wanaokutana mjini Malabo, Equatorial Guinea.
Wakuu wa nchi za Afrika na zile za kiarabu wanaokutana mjini Malabo, Equatorial Guinea. DR

Nchi ya Morocco pamoja na mataifa kadhaa ya kiarabu, wamejiondoa kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na zile za kiarabu mjini Malabo, Equatorial Guinea, wakipinga uwepo wa ujumbe kutoka eneo la Polisario (Sahara Magharibi), vyombo kadhaa vya habari vimeripoti. 

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Morocco, muwekezaji mkubwa barani Afrika, imejiondoa kwenye mkutano wa 4 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Afrika na Ghuba, ambapo inaelezwa hatua yake iliungwa mkono na Saudi Arabia, Bahrain, Qatar, Ufalme wa Oman, Jordan, Yemen na Somalia.

Ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Morocco kwenye taarifa yake imesema kuwa, ujumbe wake uliondoka kwenye mkutano huo, ukipinga uwepo wa wajumbe kutoka eneo la Polisario, ambalo Morocco inadai ni eneo lake.

Nchi ya Morocco inasema eneo la Sahara Magharibi ni sehemu ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo toka walipopata uhuru kutoka kwa wakolini wao wa zamani, nchi ya Uhispania, lakini sasa eneo hilo linataka kujitenga.

Ujumbe wa Morocco uliondoka mjini Malabo, wakati huu nchi hiyo ikijaribu kusaka uungwaji mkono ili irejeshwe kwenye umoja wa Afrika, ambapo utawala wa Rabat ulijiondoa mwaka 1984, ukipinga uamuzi wa nchi huru za Afrika wakati huo, kulitambua eneo la Polisario kuwa

Ripoti hizi zilioneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Africa 24, ambacho kinaonesha mkutano huu Mubashara.