AU-ECOWAS

Wakuu wa nchi za Afrika wanakutana Malabo na wenzao wa nchi za Ghuba

Wakuu wa nchi za Afrika na wale kutoka nchi za kiarabu za Ghuba, wanakutana mjini Malabo, Equatorial Guine, ikiwa ni mkutano wao wa 4 kati ya umoja wa Afrika na wakuu wa nchi za ki

Mwenyekiti wa ECOWAS Alassane Ouattara, ambaye leo anaongoza viongozi wengine wa kanda hiyo katika mkutano na nchi za Ghuba ya kiarabu
Mwenyekiti wa ECOWAS Alassane Ouattara, ambaye leo anaongoza viongozi wengine wa kanda hiyo katika mkutano na nchi za Ghuba ya kiarabu Reuters/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Wakuu hawa wa nchi mbali na kuzungumzia masuala ya usalama na hasa vita dhidi ya makundi ya kigaidi, pia watajadiliana kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo endelevu.

Katika mkutano wao wa mwisho uliofanyika nchini Kuwait mwaka 2013, wakuu wa nchi za Ghuba, waliahidi kulisaidia bara la Afrika kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 mpaka kufikia mwaka 2018, mpango uliokuwa chini ya mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait.

Hata hivyo safari hii, viongozi hawa wanatarajiwa kuweka mikakati ya utekelezaji wa makubaliano yao ya awali na kuangalia namna bora ya kushirikiana na kutumia rasilimali za bara la Afrika.

Kuelekea mkutano huu, kwa mara ya kwanza mawaziri wa mambo ya nje, uchumi, fedha na biashara walikutana kwa nyakati tofauti.