OIF-MADAGASCAR

Nchi tano kujiunga na OIF

Kituo kipya cha mkutano cha Ivato, Madagascar.
Kituo kipya cha mkutano cha Ivato, Madagascar. RFI/Paulina Zidi

Wakati ambapo mkutano wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa ukiingia siku yake ya pili Jumapili hii Novemba 27 mjini Antananarivo, nchini Madagascar, matangazo kadhaa yanatarajiwa kutolewa mchana wa leo ikiwa ni pamoja na jina la nchi itakayo kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi hizo mwaka 2018 na nchi mpya ambazo ziko tayari kujiunga na OIF.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu, nchi tano zimewasilisha maombi yao kujiunga katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF), lakini nne pekee tayari zimekubaliwa.

Kuanzia Jumapili hii, Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) itazipokea nchi nne mpya wanachama. Hakika, miongoni mwa nchi 5 zilizowasilisha mambi yao kujiunga na OIF, nne pekee zilikubaliwa wakati wa kikao cha siku ya Jumamosi.

Ujumbe wa kwanza uliowekwa kwenye hatma yake ni ule wa Ontario, ambayo imekubaliwa kuwa mwanachama wa OIF. Ujumbe wa Canada umepongeza hatua hiyo na kusema kwamba ni ushindi kwao. Ujumbe wa Canada katika mkutano huo walisheherekea tukio hilo, wakirusha taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Nchi ya Korea Kusini, Argentina na New Caledonia, pia wamekubaliwa kuwa wanachama wapya wa jumuiya wa nchi zinazozungumza KIfaransa (OIF).

Hata hivyo, Saudi Arabia haikukubaliwa ombi lake kutokana na kwamba faili yake haikamiliki. Ombi la Saudi Arabia kujiunga katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa limeahirishwa kwa mkutano wa kilele ujao mwaka 2018 na ombi hilo litajadiliwa kabla kufanyiwa uchunguzi na jopo la OIF.