DRC-MAUAJI-USALAMA

Raia 35 wauawa katika shambulio la wanamgambo wilayani Lubero

Askari wa Umoja wa Mataifa kutoka India wakipiga doria katika msitu wa Pitakongo, wilayani Lubero, mkoani Kivu Kaskazini, Novemba 10, 2014.
Askari wa Umoja wa Mataifa kutoka India wakipiga doria katika msitu wa Pitakongo, wilayani Lubero, mkoani Kivu Kaskazini, Novemba 10, 2014. Photo : Force/MONUSCO

Raia thelathini na tano na mwanamgambo mmoja kutoka kundi la Mai Mai waliuawa Jumapili Novemba 27 katika shambulizi la wanamgambo katika kijiji cha Luhanga, wilayani Lubero, katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

dadi hii imetolewa na vyanzo vya mashirika ya kiraia wilayani Lubero Mkuu wa wilaya hiyo, Bokele Furaha.

Vyanzo hivyo vinaripoti kwamba wanamgambo wa Mai Mai walishambulia wilaya ya Luhanga mapema asubuhi kati ya saa 10:00 na saa 11:00 alfajiri.

Akihojiwa na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya ya Lubero alisema kuwa washambuliaji waliendesha shambulizi hilo baada ya kugundua kuwa idadi ya wanajeshi ilikua ndogo mno.

"Walianza kushambulia ngome ya jeshi la FARDC (jeshi la DRC). Wakati walipokua wakishambuliwa askari wa FARDC, kundi jingine lilikua likiwaua raia kwa visu au risasi, " amesema Bw Bokele, akiwasiliana na shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kutoka Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Ukiukaji wa sheria za kimataifa

Kwa upande wake shirika lisilo la kiserikali la CEPADHO, limesema kuwa shambulio hilo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.