DRC-CHINA-USHIRIKIANO

Ardhi iliyopewa China yazua utata nchini DRC

rRaia waandamana mjini Kinshasa,Septemba 19, 2016.
rRaia waandamana mjini Kinshasa,Septemba 19, 2016. AFP/EDUARDO SOTERAS

Zaidi ya wanafunzi 300 wa Chuo kikuu cha Gombe wamefanya maandamano Jumatatu hii katika mji wa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) dhidi ya hatua ya serikali ya kuupa ubalozi wa China sehemu ya ardhi.

Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Gombe, kaskazini mwa mji wa Kinshasa, waliingia mitaani kuanzia saa 1:00 asubuhi saa za kimataifa, huku wakiimba nyimbo zinazopinga China.

Waandamanji hao walizuia barabara inayoelekea kwenye makao makuu ya Wizara ya Elimu, katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Kwa mujibu wa afisa wa Wizara ya Elimu aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP,ardhi hiyo ilipewa ubalozi wa China nchini DRC, ambayo itajenga kituo cha data.

hatua hii ya serikali ya kuupa ubalozi wa china sehemu hiyo ya ardhi imesababiha hali ya taharuki, kwa sababu, kwa mujibu wa wanafunzi, Chuo kikuu cha Gombe kilinyang'anywa vifaa kadhaa ikiwa ni pamoja na bwawa la kuogelea na uwanja wa michezo.

Sehemu hizo, inaaminika kuwa, kwa mujibu wa wanafunzi hao zinamilikiwa kwa sasa na ndugu wa Rais Joseph Kabila.