Habari RFI-Ki

Kauli ya CENI nchini DRC kuhusu uchaguzi mwaka 2017

Sauti 10:07
Mwenyeki wa Tume huru ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa  Yobeluo akihojiwa na wandishi wa habari jijini Kinshasa
Mwenyeki wa Tume huru ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa Yobeluo akihojiwa na wandishi wa habari jijini Kinshasa MONUSCO/Alain Wandimoyi

Mwenyekiti wa tume huru ya Uchaguzi nchini DRC Corneille Nangaa amesema tume yake iko tayari kuandaa uchaguzi katika mwaka 2017 ikiwa itawezeshwa.Akizungumzia uwezekano huo kwenye ofisi kuu ya Seneti, Nangaa amesema tume ya uchaguzi ina uwezo wa kuandaa uchaguzi katika hali ya utulivu, na kwamba Julai 31 mwaka ujao watakuwa wamemaliza kuwaandika wapiga kura, hivyo kuna uwezekano wa kuitisha uchaguzi Oktoba 30, 2017.