DRC-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea Tshikapa baada ya siku mbili za mapigano makali

Tshikapa, mji mkuu wa Kasai-Central ulishuhudia mapigano makali mwishoni mwa wiki hii iliyopita.
Tshikapa, mji mkuu wa Kasai-Central ulishuhudia mapigano makali mwishoni mwa wiki hii iliyopita. Google Maps

Hali ya utulivu imerejea katika mji wa Tshikapa, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya siku mbili za mapigano makali kati ya wanamgambo na vikosi vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la DRC, FARDC, limesema mgogoro wa kimila ulizuka katika mji huo na kusababisha hali ya taharuki, na wasiwasi kwa wakazi wa mji huo.

Kwa mujibu wa vyanzo vingine katika mji huo, kundi la wanamgambo wa kiongozi mkuu Kamwina Nsapu aliyeuawa kwa risasi katika wilaya ya Dibaya wiki kadhaa zilizopita ndio chanzo cha mgogoro huo.

Taarifa ya serikali imebaini kwamba mgogoro wa madarakaza ya kimila katika eneo la Mbawu ndio chanzo cha kuzorota kwa usalama. Naibu Mkuu wa mkoa wa Kasai-Central alikuwa wa kwanza kusema hilo, Mkaguzi Mkuu wa Majeshi alirejelea kauli hiyo katika taarifa ya Jumapili usiku iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa. Na jenerali Ponde aliongeza kuwa wapiganaji wanaozuliwa na vikosi vya usalama watafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi ambapo watashitakiwa pia kutumia watoto katika kundi la wanamgambo wenye silaha.

Kwa mujibu wa vyanzo katika mji wa Tshikapa, washambuliaji walikua wakidai kuwa ni wanamgambo wa Kamwina Nsapu, kiongozi wa kimila ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi wiki chache zilizopita na polisi katika mji wa Dibaya, katika mkoa jirani wa Kasai Central. Katika harakati zao kutokamji wa Mbawu hadi mji wa Tshikapa, kundi hili wanamgambo lilikua likikabiliana na polisi. pande zote mbili zilipoteza watu wao. Miongoni mwa waathirika, watoto walijikuta wakipigwa risasi hewa.

Machafuko hayo yalianza siku ya Ijumaa na hali hiyo ilienea Jumamosi. Hali ya utulivu ilirudi Jumapili mchana baada ya jeshi kuingilia kati.