NIGERIA-UN

Nigeria: Umoja wa Mataifa unakuza habari kuhusu njaa

Wanawake wakikusanya katika kambi ya wakimbizi wa ndani mjini Abuja, Nigeria Oktoba 3, 2016.
Wanawake wakikusanya katika kambi ya wakimbizi wa ndani mjini Abuja, Nigeria Oktoba 3, 2016. REUTERS/Afolabi Sotunde

Ofisi ya rais nchini Nigeria inasema kwamba mashirika ya misaada ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa wanakuza habari kuhusu hali ya njaa kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa rais wa Nigeria Garba Shehu amesema Jumanne hii kuwa "madai yasiyokua na msingi" yalifanywa na mashirika ya misaada yanayoendesha harakati zao katika ukanda huo.

Umoja wa Mataifa unasema baadhi ya watoto 75,000 wako katika hatari ya njaa katika miezi ijayo.

"Tuna wasiwasi kwa majaribio ya wazi ya kuchochea wasiwasi usiokepo kuhusu njaa, kitendo kinachofanywa na baadhi ya mashirika ya misaada ya kimataifa," amesema afisa wa Nigeria alyeinukuliwa na shirika la habri la Reuters.

Shehu anasikitishwa na kuona mashirika hayo yanaweka mbele maslahi yao kwa kuweza kusaidiwa kifedha kuliko kutafuta suluhu kwa suala hilo.

Amekumbusha kwamba hivi karibuni "shirika moja la Umoja wa Mataifa lilitoa onyo kwa raia na jumuiya ya kimataifa kwamba mwaka ujao watu 100,000 watakufa kutokana na njaa. Shirika jingine lilisema kuwa watu milioni moja watafariki."

Siku ya Ijumaa, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa uliongeza mara mbili misaada yake ya kibinadamu kwamwaka 2017 kwa mikoa ya Kaskazini Mashariki ya Nigeria (dola bilioni 1), ambapo, karibu watu milioni 7 walisema wanahitaji msaada muhimu.

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) limesema kuwa liliandaa mpango "kwa ushirikiano wa karibu na Serikali."