MANDELA-AFRIKA KUSINI

Raia Afrika Kusini waadhimisha miaka 3 toka kifo cha Nelson Mandela

Mkazi wa Soweto akiangazia kwa mshumaa picha ya Nelson mandela iliyochorwa kwa rangi , Desemba 4 mwaka 2014.
Mkazi wa Soweto akiangazia kwa mshumaa picha ya Nelson mandela iliyochorwa kwa rangi , Desemba 4 mwaka 2014. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Dunia pamoja na wananchi wa Afrika Kusini, hii leo wanafanya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kifo cha muasisi wa taifa hilo na rais wa kwanza mweusi baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi, Nelson Madiba Mandela.

Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho haya yanafanyika wakati huu nchi ya Afrika Kusini ikipitia kipindi kigumu cha kiuchumi na kisiasa, hasa kutokana na kashfa za rushwa zinazokiandama chama tawala cha ANC.

Maadhimisho haya yanafanyika huku wakosoaji wa rais Jacob Zuma, wakimtuhumu kwa kushindwa kuenzi yale aliyoyapigania muasisi huyo ndani ya chama, hasa linapokuja suala la rushwa serikali.

Wakati chama tawala kikipitia wakati mgumu, uchumi wa taifa hilo umeendelea kuzorota, huku wananchi wa kijiji Qunu, alikozaliwa muasisi huyo wakilalama kuhusu hali mbaya ya maisha toka yalipofanyika mazishi ya kiongozi huyo.

Mamia ya raia wanatarajiwa kufika kijijini Qunu, kufanya ibada kumkumbuka musasisi huyo aliyefariki December 5, mwaka 2013.