MALI-USALAMA

Mali: wafungwa wa gereza la Niono watoroka baada ya shambulio

Askari wa Mali karibu na kambi ya jeshi katika mji wa Niono, katikati mwa nchi  ya Mali, mwezi Januari 2013.
Askari wa Mali karibu na kambi ya jeshi katika mji wa Niono, katikati mwa nchi ya Mali, mwezi Januari 2013. AFP PHOTO / FABIO BUCCIARELLI

Nchini Mali, usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, gereza la Niono. lililoko katikati mwa jimbo la Segou, katikati mwa Mali, lililengwa na shambulio. Washambuliaji walivamia majengo ya gereza hilo. Waliwajeruhiwa askari magereza wawili kabla ya kufyatua risasi kwenye mlango na kufunguka na kupelekea wafungwa wengi kutoroka.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, washambuliaji walikuja katika gereza hilo kwa gari na pikipiki.

Baadhi waliwasili katika gereza hilo wakivalia sare za kijeshi, wengine wakivalia mavazi ya kawaida na kuvamia majengo ya gereza la Niono, huku wakisema kwa sauti ya juu "Allah Akbar". Inaonekana kuwa walikua walikuja kwa lengo moja tu la kuwatorosha wafungwa wawili au mmoja. Washambuliaji hao walitumia fursa hiyo kwa kuacha wazi lango na kuwatorosha wafungwa wengine. Takriban wafungwa 90 waliweza kutoroka, kwa mujibu wa mwakilishi wa wizara ya Ulinzi. Baada ya kutoroka kwao, kundi dogo lilirejea katika jela, kwa hiari au kwa nguvu.

Operesheni ambayo bado inazua maswali mengi ya usalama wa magereza na ya nchi ya Mali. Mbunge Belco Bah anaamini kwamba eneo la Niono ni kubwa sana na ni vigumu kulitolea ulinzi. afisa mmoja wa serikali za mitaa amebaini kwamba uwezo wa kijeshi hautoshi dhidi ya mashambulizi ya kuvizia.

Jela la Niono linashambuliwa kwa mara ya pili kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja.