SOMALIA-IS-USALAMA

IS yatimuliwa katika eneo la Puntland

Askari wa Somalia wakipiga doria katika mkoa wa Puntland.
Askari wa Somalia wakipiga doria katika mkoa wa Puntland. AFP PHOTO / Mohamed Abdiwahab

Baada ya siku kadhaa za mapigano, serikali ya mkoa unaojitegemea wa Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia, ilitangaza Jumatano, Desemba 7 kwamba imeudhibiti mji wa bandari wa Qandala uliokuwa kwa wiki kadhaa mikononi mwa wanajihadi wanojidai kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama vilishambulia, baada ya siku 11 vikitembea katika mazingira magumu katika njia ya ardhini, na njia ya bahari kutoka Ghuba ya Aden. Lakini hapakuwa na mapigano. Kwa sababu, wanajihadi hawakujibu mashambulizi hayo, kwani wengi wao tayari walikua wameshaondoa katika mji huo.

Kwanza kulikua na makabiliano makali alikuwa vurugu na mapigano, Jumamosi na Jumatatu, Jumamosi na Jumatatu, huku ndege zisizo kuwa na rubani za Marekani zilisaidia, na hatimaye kulikua na mazungumzo kati ya serikali na ukoo mkubwa katika mkoa huo, ukoo anakotoka kiongozi wa kundi la Islamic State katika mkoa huo, Abdulqadir Mumin.

Mji wa Qandala ulikuwa kwake kama ishara ya kukamatwa ambao ungelitumika kwa propaganda yake, lakini mji huo pia ungelitumia kwa makundi mengine ya kigaidi.

Kundi hili liliwapoteza wapiganaji wake zaidi ya thelathini, kwa mujibu wa serikali ya Puntland, ambayo imewatolea wito wakazi wa mkoa huo kurudi nyumbani, kwani hali ya usalama imedhibitiwa vikosi vya usalama.

Hata hivyo, serikali ya Puntland haina uhakika kwamba wito huo utaitikiwa kwani, wanajihadi waliokimbia hawako mbali sana. Walikimbilia katika milima, kilomita kumi tu kutoka mji wa Qandala.