GAMBIA

Yahya Jammeh apinga matokeo ya uraisi juma moja tangu akubali kushindwa

Raisi wa Gambia Yahya Jammeh
Raisi wa Gambia Yahya Jammeh

Raisi wa Gambia Yahya Jammeh ambaye juma lililopita alimpigia simu mpinzani wake Adama Barrow akimpongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo,ameyakataa matokeo hayo na kudai kutoyatambua.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika televisheni ya taifa nchini Gambia raisi anayemaliza muda wake Yahya Jammeh amesema kwa namna ile ile ambayo aliyapokea matokeo akiamini tume ya uchaguzi ilikuwa huru na ilitenda haki sasa anayakataa matokeo hayo kabisa.
Kiongozi huyo alisistiza kuwa hakubali matokeo hayo kulingana na makosa yaliyopo ambayo hayakubaliki kwa upande wa tume ya uchaguzi na kutoa wito wa uchaguzi kurudiwa.

Awali raisi mteule Barrowa alisema kuwa aliambiwa na rais anayemaliza muda wake, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa urais, Yahya Jammeh, kwamba anapendelea kubaki nchini Gambia na kuendelea kujihusisha na mifugo yake katika kijiji alikozaliwa. Tunapaswa kumuondolea mashaka, amesema Rais adama Barrow.

Lakini sasa bado haijulikani msimamo wa Adama baada ya kauli ya jammeh.