MISRI-USALAMA

Misri yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 3

Shambulizi liliendeshwa dhidi ya kanisa la Coptic mjini Cairo, Desemba 11, 2016.
Shambulizi liliendeshwa dhidi ya kanisa la Coptic mjini Cairo, Desemba 11, 2016. REUTERS/Amr Abdallah

Misri imetangaza siku tatu ya maombolezo baada ya kutokea kwa mlipuko ndani ya Kanisa la Coptic na kusababisha vifo vya watu 25. Kanisa hili sio mara ya kwanza kukumbwa na mkasa huo wa mashambulizi

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi katika Kanisa hilo kuu, limezua hasira kubwa jijini Cairo.
Mamia ya Wakiristo na Waislamu waliandamana siku ya Jumapili, Desemba 11 kulaani kitendo hicho ambacho kimesababisha vifo hivyo wengi wakiwa watoto na wanawake.

Waandamanaji hao wamemshtumu rais Abdel Fattah el-Sisi kwa shambulizi hilo na kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Magdy Abdel Ghaffar, kwa madai ya kushindwa kudumisha usalama hasa katika kanisa hilo.

Walinzi wa Kanisa hilo wamedaiwa kuwa wakati wa shambulizi hilo walikuwa wakijihusisha na michezo ya Mitandao na hivyo hawakuwa makini.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kanisa la Coptic nchini Misri kushambuliwa, tangu mwaka 2011 wakati kiongozi wa zamani wa nci hiyo Hosni Mubarak alipoondolewa madarakani.

Asilimia 10 ya raia wa Misri ni waumini wa dhehebu hilo.