GAMBIA-UN-SIASA

Ibn Chambas: Jammeh apaswa kuondoka madarakani mwezi Januari

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, alisema Jumatano kuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema "kuwa tayari kukabidhi madaraka" mwezi Januari.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, alisema Jumatano kuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema "kuwa tayari kukabidhi madaraka" mwezi Januari. AFP

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, amesema Jumatano hii kuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh anapaswa "kuwa tayari kukabidhi madaraka" mwezi Januari mwakani.

Matangazo ya kibiashara

Bw ibn Chambas amesema Umoja wa Mataifa hautaendelea kufumbia macho viongozi ambao hushindwa na kisha baadaye wanatumia nguvu kwa kuchukua madaraka.

"Upinzani ulishinda uchaguzi, ambao halali" amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa wa Ban Ki-moon katika Afrika ya Magharibi.

Jumanne wiki hii Marais wanne kutoka Afrika Magharibi walifanya ziara katika mji mkuu wa Gambia, Banjul na kujaribu kumshawishi Yahya Jammeh kukubali kushindwa katika uchaguzi wa urais na kukabidhi madaraka, bila mafanikio.

Mihula ya miaka mitano ya Bw Jammeh itamalizika Januari 19, Mohamed Ibn Chambas amesema, huku akiongeza kuwa "atakuwa tayari kukabidhi madaraka" tarehe hiyo.

"Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki majukumu yake yatakua sambamba na Katiba," amesema afisa huyo wa Umoja wa Mataifa.

Kuhusu rufaa ya Bw Jammeh kwa Mahakama, Mohamed Ibn Chambas amehakikisha kwamba masuala hayo mawili hayana uhusiano wowote.

"Utaratibu huu wa kisheria hauhusiani na kumalizika kwa muhula wake," ambao utamalizika mwezi Januari, Bw Ibn Chambas amesema.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani hatua ya jeshi kudhibiti Tume ya Uchaguzi na kuwafukuza wafanyakazi wote ambao kwa sasa hawawezi kwenda kazini.

Moon amemtaka rais Jammeh kuamuru wanajeshi hao kuondoka katika tume hiyo mara moja.

Rais Mteule Barrow, naye ameendelea kushinikiza Yahya Jammeh aondoke madarakani wakati huu chama chake kikiwa kimekwenda Mahakamani kupinga matokeo ya Uchaguzi wa tarehe moja mwezi