SUDAN KUSINI

Machar apewa kifungo cha nyumbani nchini Afrika Kusini

Maafisa wa Afrika Kusini wamethibitisha kuwa, kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar amepewa kifungu cha nyumbani ili kumzuia kuondoka nchini humo.

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar
Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar AFP Photo:UNMISS/Isaac Alebe Avoro
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja baada ya Machar kufanikiwa kwenda jijini Khartoum nchini Sudan na Addis Ababa nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi uliopita bila ya kibali maalum kutoka kwa serikali ya Pretoria.

Ripoti ya Shirika la Habari la Reuters inasema, Machar ataendelea kuwa nyumbani kwake jijini Pretoria na mawasiliano ya simu zake yatachunguzwa.

Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Clayson Monyela amekanusha madai hayo na kusema Machar ni mgeni wa Afrika Kusini, na amepewa hifadhi ili kuepuka machafuko nchini mwake.

Mwezi Agosti mwaka huu, baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa nchi za Afrika Masharii IGAD, ilikubaliwa kuwa Machar aendee nchini humo ili kuepuka machafuko zaidi katika nchi yake.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa nchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na hatari ya kutokea kwa mapigano ya kikabila.