DRC-UNSC

Mazungumzo ya kumaliza mzozo DRC kuendelea jumatano

Raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo,DRC Joseph Kabila
Raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo,DRC Joseph Kabila REUTERS/Tiksa Negeri

Mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kabla ya kumalizika kwa muhula wa rais Joseph Kabila, yamesitishwa hadi jumatano ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa maaskofu wanaosimamia mazungumzo hayo CENCO Marcel Utembi amesema mazungumzo hayo yamesitishwa.

Tangazo hilo lilikuja baada ya mazungumzo yaliyofanyika jumamosi kati ya chama tawala chake Joseph kabila na makundi ya upinzani kusaka suluhu kwa taifa la Drc baada ya decemba 20 muhula wa raisi Kabila utakapokoma.

Wadau, wawakilishi na wafuasi wa chama tawala, upinzani na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki, CENCO, ambao ndio wapatanishi wakuu, walikutana kuanzia saa tano Asubuhi Desemba 17.

Mazungumzo haya yalianzishwa Desemba 8 na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki, yalikuwa yamalizike Ijumaa ya Desemba 16, lakini yalilazimika kusogezwa mbele kwa siku moja zaidi baada kukosekana kwa makubaliano na muungano mkuu wa upinzani.