SENEGAL-Ufaransa

Macky Sall aanza ziara ya kikazi nchini Ufaransa

Macky Sall azuru Ufaransa.
Macky Sall azuru Ufaransa. Source : mycitypapers.com

Rais wa Senegal Macky Sall aliwasili Jumapili jioni katika mji wa Paris, nchini Ufaransa, kwa ajili ya ziara ya kikazi, ziara ya kwanza baada ya ile ya Abdou Diouf mwaka 1992.

Matangazo ya kibiashara

Bendera za nchi hizi mbili zimepandishwa kwenye ofisi mbalimbali za serikali hasa katika Ikulu ya Champs-Elysées, kwenye manispaa ya jiji la Paris na majengo makubwa ya mji mkuu wa Ufaransa.

Leo Jumatatu, Rais wa Senegal atazuru kampuni ya Alstom mjini Strasbourg. Kampuni hii inayotengeneza treni ilisaini hivi karibuni mkataba na kampuni ya Senegal ya TER ambayo itasimamia ujenzi wa uwanja mpya wa kimataifa wa ndege mjini Dakar .

Jumanne wiki hii, Bw Sall ataendelea na ziara yake, ambapo atazuru eneo waliko zikwa askari waliosaidia Ufaransa katika vita vya pili vya dunia, na kisha atakutana kwa mazungumzo na rais François Hollande, huku wakiwepo rais wa baraza la Seneti na Spika wa Bunge, na baadaye atafanyiwa mahfali katika ukumbi wa manispaa ya jiji la Paris kabla ya kula chakula cha jioni kiliyoandaliwa na serikali ambapo watashiriki viongozi wa serikali wa Senegal na wenyeji wao, katika Ikulu ya Elysée.

Ziara hii itakuwa fursa kwa Senegal kuonyesha uwezo wake, utamaduni wake, ukuaji wake, lakini pia kukumbusha baadhi ya mikataba.