LIBYA-MAREKANI-IS-USALAMA

Marekani yasitisha operesheni zake za kijeshi katika mji wa Sirte

Marekani inasema jeshi lake limemaliza operesheni katika ngome ya zamani ya kundi la Islamic State nchini Libya, mjini Sirte. Hali imeendelea kutisha katika mji huo ambao baadhi ya maeneo yake yanaendelea kushikiliwa na kundi la IS, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Libya.

Mpiganaji wa vikosi vinavyotii serikali mpya ya Umoja nchini Libya akichunguza eneo la kundi la Islamic State katika eneo la Algharbiyat katika mji wa  Syrte, Juni 21, 2016.
Mpiganaji wa vikosi vinavyotii serikali mpya ya Umoja nchini Libya akichunguza eneo la kundi la Islamic State katika eneo la Algharbiyat katika mji wa Syrte, Juni 21, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia mwezi Agosti jeshi la Marekani limekuwa likipambana na wapiganaji hao katika mji wa Sirte ili kuukomboa na kuisaidia serikali inayotambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa.

Ni miaka kadhaa sasa nchi ya Libya ikikabiliwa na mdodroro wa usalama , huku mapigano kati ya makundi hasimu yakishuhudiwa, ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State lililokua likiendesha harakati zake katika mji wa Sirte.

Hata hivyo hali ya usalama katika mji wa Sirte bado inatisha, kufuatia mashambulizi ya kuvizia na mapigano ya hapa na pale.

Raia wengi wamepoteza maisha kufuatia vita vilivyozuka katika mji huo pamoja na mashambulizi ya kuvizia yanayoendeshwa na makundi mbalimbali, hasa kundi la Islamic State dhidi ya vikosi vya usalama.