Wafanyakazi wa shirika la ndege la Arik Air wasitisha mgomo wao

Maelfu ya abiria walikwama baada shirika la ndege la Arik Air, shirika kubwa la ndegenchini Nigeria, kutangaza Septemba 13 kuwa limesitisha kwa muda safari zote za ndege.
Maelfu ya abiria walikwama baada shirika la ndege la Arik Air, shirika kubwa la ndegenchini Nigeria, kutangaza Septemba 13 kuwa limesitisha kwa muda safari zote za ndege. Crédit : Biggerben/Wimedia Commons

Safari za ndege za Shirika la Arik Air, zimeanza tena nchini Nigeria baada ya mgomo wa siku moja. Wafanyakazi wa Arik waliitisha mgomo wa siku moja, kulalamikia kutolipwa mshahara kwa muda wa miezi saba.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya uongozi wa Shirika hilo kutangaza kuwa limepata mwafaka kat yao na wafanyikazi wa Shirika hilo la ndege.

Wafanyakazi wa Arik waliitisha mgomo wa siku moja, kulalamikia kutolipwa mshahara kwa muda wa miezi saba lakini pia kulalamikia hatua ya kufutwa kazi kwa wenzao watano.

Pamoja na mwafaka huo, Shirika hilo pia limesema litanunua ndege kubwa ili kusafirisha idadi kubwa ya abiria.

Imekubaliwa kuwa, wafanyakazi wa shirika hilo watalipwa mshahara wao kufikia tarehe 31 mwezi huu na ikiwa ahadi hiyo haitatekelezwa, watarejelea mgomo wao.

Arik Aire ndilo Shirika kubwa la ndege nchini Nigeria zikiwa na safari kwenda jijini Johannersbug nchini Afrika Kusini na New York Marekani.