CONGO-LIBYA-MAREKANI

Sassou-Nguesso ziarani Marekani kukutana na Donald Trump

Denis-Sassou Nguesso, rais wa Congo-Brazzaville, Machi 3, 2015 wakati wa ziara yake mjini Brussels.
Denis-Sassou Nguesso, rais wa Congo-Brazzaville, Machi 3, 2015 wakati wa ziara yake mjini Brussels. AFP/Thierry Carlier

Taarifa kutoka Ofisi ya rais wa Congo-Brazzaville imetangaza kuwa rais wa nchi hiyo, Denis Sassou-Nguesso, atapokelewa na Donald Trump. Rais wa Congo akutana Jumanne hii Desemba 27 na rais mteule wa Marekani, kujadili rasmi mgogoro wa Libya. Denis Sassou-Nguesso ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Umoja wa Afrika kwa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii imepangwa hasa kutafutia njia za kuondoa Libya katika mgogorounaoikabili kwa miezi kadhaa. Majadiliano pia yatalenga maeneo mengine ya bara la Afrika na masuala ya kimataifa, kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya rais Denis Sassou-Nguesso

Lakini kwa upande wa upinzani Congo, unaopinga mpaka sasa uchaguzi wa Denis Sassou-Nguesso mwezi Machi, mkutano huoi, ingawa si ziara ya kiserikali, Inaleta picha mbaya kwa Congo, kwa mujibu wa Charles Zacharie Bowao, msemaji wa chama cha upinzani

"Tungelipenda achukuliye hali inayojiri nchini Libya ili aweze kupata fundisho. Kuweka mikakati ya kuelekea katika uimarishaji wa demokrasia, kuheshimu haki za binadamu, kuheshimu vyombo vya sheria. Kama amekwenda kuidhinisha serikaliambayo ilipoteza uhalali wote, ni wazi kwamba ziara yake haituhakikishii chochote, amesema Bw Bawao. Hatujui nini watafikia, lakini ni ujumbe mbaya. "

Akihojiwa na RFI, Waziri wa Mawasiliano wa Congo Thierry Moungala amesemakwamba Donald Trump ana shauku ya kujua ukweli kuhusu hali inayojiri nchini Libya na kwingineko barani Afrika. Bw Moungala ameongeza kuwa si tukio la kuwa wa kiongozi wa kwanza au wa mwisho kukutana na Donald Trump.