DRC-JOSEPH KABILA

Makubaliano ya kihistoria yatiliwa sahihi DRC kumaliza mzozo wa kisasa

Mkuu wa Maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC wanaosimamia mazungumzo ya kisiasa Marcel Utembi
Mkuu wa Maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC wanaosimamia mazungumzo ya kisiasa Marcel Utembi AFP/JUNIOR D.KANNAH

Hatimaye Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC na vyama vya siasa vimeitiliana saini makubaliano rasmi juu ya hatma ya raisi Joseph Kabila,na kumaliza mzozo wa kisiasa uliosababisha miezi kadhaa ya ghasia.

Matangazo ya kibiashara

Chini ya masharti ya makubaliano hayo raisi Kabila atasalia madarakani hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2017 lakini baraza la serikali ya mpito litaundwa na kuongozwa na kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi.

Aidha waziri mkuu atateuliwa kutoka upande wa upinzani.

Mazungumzo hayo yaliratibiwa na kanisa katoliki wakati raisi Kabila akitamatisha muda wake kuwepo madarakani dec 20 bila kuwa na dalili za kuachia kiti cha uraisi wala utayari wa kufanya mchakato wa uchaguzi.

Makubaliano ya mwisho yalitiliwa saini baada ya masaa 13 ya majadiliano hapo jana jumamosi.